Muigizaji mr Ibu aeleza kukatwa miguu, Aomba msaada

Muigizaji mr Ibu aeleza kukatwa miguu, Aomba msaada

Muigizaji mkongwe kutoka nchini Nigeria, John Ikechukwu, maarufu kama Mr Ibu ameweka wazi kuwa anapambana na ugonjwa unaotishia maisha yake huku akiwaomba watu kumsaidia pesa kwa ajili ya matibabu.

Kupitia ukurasa wa Instagram ame-share video hiyo akizungumza akiwa hospitalini kwa kuomba msaada kwa mashabiki wake waweze kumchangia na kufichua kuwa kufuatia ugonjwa alionao huenda ukasababisha kukatwa miguu.

Mwaka 2022, aligunduliwa na ugonjwa wa kisukari na figo na alifanyiwa upasuaji katika kituo cha matibabu na figo cha Zenith huko Abuja.

Mr Ibu aliacha kushiriki katika kazi za Sanaa kwa sababu ya ugonjwa huku mwaka 2019 kufuatia moja ya mahojiano yake alieleza kuwa aliwahi kuwekewa sumu kwenye chakula na watu wa kijijini kwako kwa sababu ya wivu wa mafanikio yake.

Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia movie zake kama The Collaborator akiwa na Aki na Ukwa, Mr Ibu, My Chop Money nk.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags