Mtu mrefu zaidi duniani alivyoteseka na mapenzi

Mtu mrefu zaidi duniani alivyoteseka na mapenzi

Sultan Kosen ambaye ni mkulima kutoka nchini Uturuki kwa sasa ndiye anashikilia rekodi ya kuwa mwanadamu mrefu zaidi duniani.

Kosen ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 41 anatajwa kuwa ndiye mwanadamu mrefu zaidi ambapo kwa mujibu wa rekodi za dunia za vitabu vya  Guinness, imeelezwa kuwa ana urefu wa futi 8 na inchi 2+7⁄8.

Mbali ya urefu wa mwili wake pia anashikilia rekodi ya kuwa mwanadamu mwenye mikono mirefu zaidi ambayo inafikia sentimita 28.

Moja ya changamoto ambazo  mwanaume huyu anadai kuwa alikuwa anapitia ni wanawake wengi kumuogopa hivyo  hadi anafikia umri wa miaka 26 ambapo ndiyo aliingia rasmi kwenye rekodi ilikuwa ngumu kwake kupata mchumba.

"Ni ngumu sana kupata mchumba, kawaida huwa wananiogopa, nina matumaini kwamba sasa nimekuwa maarufu wasichana wengi wanaweza kujitokeza na nikatimiza ndoto yangu na kufunga ndoa." alisema Sultan mwaka 2009 alipokuwa anahojiwa na tovuti ya guinness World Record.

Baada ya hapo Sultan alimuoa mrembo Merve Dibo mwaka 2013 na akaachana naye mwaka 2021.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags