Mtoto wa Wolper gumzo mitandaoni

Mtoto wa Wolper gumzo mitandaoni

Eee bwana mtu wangu wa nguvu leo kwenye gumzo mitandaoni moja ya stori iliyobamba ni ya mtoti wa Star wa filamu na mkali wa fashion stylist nchini Tanzania, Jacqueline Wolper maarufu kama wolperstylish, jana kupitia mkutano na waandishi wa habari amemuonesha mtoto wake kwa mara ya kwanza.

Wolper ambaye pia ametaja jina kamili la Mtoto wake kuwa ni Paschal, ambapo yeye na Baba Mtoto wake wamesema Sababu ya kumpa jina hilo ni kwakua amezaliwa katika sikuku ya Pasaka.

Pia walimtangaza mtoto huyo kuwa balozi wa nguo na bidhaa za watoto kwenye duka maarufu la SweetLorah linalojihusisha na uuzaji wa vitu vya watoto kama nguo, viatu na vitu vingine.

Unaambiwa kuwa mtoto huyo amezua gumzo katika mitandao huku wengi wao wakisema amefanana na mama yake mzazi kuliko baba yake.

Tuambie na wewe unadhani mtoto huyo kafanana na nani, tupia maoni yako katika ukurasa wetu wa Instagram ambayo ni @mwananchiscoop.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags