Mtoto wa wakimbizi aliyekataa shule, anayesumbua EPL

Mtoto wa wakimbizi aliyekataa shule, anayesumbua EPL

Duh! Another weekend!! kama kawaida katika michezo hatuna muda wa kupoteza mapema tunakusogezea yaliojiri katika burudani na michezo na kama kawaida yetu tunakupa zile za uvunguni kabisa.

Leo katika Burudani nimekusogezea mwanasoka maarufu aliepitia katika klabu mbalimbali alizo wahi kuzichezea ulimwengu wa soka na wengi wanamtambua kutokana na mafanikio kadha wa kadha si mwengine ni Alexandre Isak.

Mmoja kati ya wachezaji waliowaka sana kwenye klabu ya Newcastle ni kiungo wa Alexandre Isak ambaye alifunga mabao mengi zaidi

Hadi sasa amefunga jumla ya mabao 10 kwenye mechi 16 za ligi Kuu England alizocheza tangu ajiunge na Newcastle katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Wakati anasajiliwa na Newcastle akitokea Real Sociedad kulikuwa na timu nyingi kubwa nchini England zilizoonyesha nia ya kumsajili lakini ziliangukia pua, hapa tumekuletea kwa undani historia na chimbuko la staa huyu.

ASILI YAKE

Huwezi kubisha hata ukimuangalia kwa sura, taarifa zinaeleza kwamba wazazi wa staa huyu ni wakimbizi kutoka nchini Eritrea ambao walizamia barani Ulaya kwa ajili ya kutafuta maisha.

Mbali ya kuzaliwa Solna huko nchini Sweden na kupewa uraia wa Sweden, staa huyu pia ana uraia wa Eritrea ambao ameupata kutokana na asili ya baba na mama yake.

Isak ambaye alizaliwa Septemba, 29, 1999. Alipokuwa mdogo alipelekwa kwenye shule moja wapo nchini Sweden kwa ajili ya kusoma lakini jambo hili halikuonekana kuwa kichwani mwake.

Suala la kusomeshwa halikuwa gumu kwa sababu nchini Sweden kuanzia elimu ya chekechea hadi chuo kikuu ni bure, hivyo licha ya hali ngumu ya wazazi wake waliweza kumpeleka shule.

Isak alikataa shule akawa anawaambia wazazi wake kwamba yeye ndoto yake ni kuwa mchezaji mpira siku moja wala sio kusoma.

Licha ya wazazi kumpinga lakini Isak alisimama kwenye maono yake hadi akaenda kufanya majaribio kwenye timu za vijana za AIK akiwa na umri wa miaka sita tu.

Aliendelea kufanya vizuri akiwa kwenye timu za vijana hata akapandishwa kwenye timu kubwa mwaka 2016, na akiwa hapo ilimchukua mwaka mmoja tu maskauti kutoka Borussia Dortmund kuona uwezo wake na akapata dili  la kujiunga na timu hiyo.

Mwenyewe anasimulia kwamba ulikuwa ni uamuzi mgumu kuondoka Sweden kuelekea Ujerumani ukizingatia alikuwa amezoea sana mazingira ya Sweden alikuwa anakwenda Ujerumani ambako hakuwa na ndugu, rafiki wala jamaa tena kwa wakati huo bado alikuwa mdogo.

KOCHA TUCHEL ALIVYO MKATAA

Wakati anatua Dortmund ilikuwa ni mpango wa timu hiyo kutafuta vipaji, hivyo kusajiliwa kwake kulitegemea ripoti ya maskauti zaidi kuliko mahitaji ya kocha.

Alipoingizwa kwenye timu kocha wa Dortmund kwa wakati huo alikuwa Tuchel naye hakuonyesha kabisa mpango wa kumuamini na kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza.

Hatimaye akaomba kuondoka kwa mkopo ambapo alisajiliwa na Willem ya Uholanzi ambapo alicheza kwa miezi sita akafunga mabao 19 na kutoa asisti tisa kwenye mechi 29.

Baada ya msimu kumalizika bado Tuchel hakuonyesha kumuamini na mwishowe Isak akaamua kujiunga na Real Sociedad ambako aliamini angepata nafasi zaidi ya kucheza, usajili wake uligharimu Euro 15  milioni.

Maisha yalimnyookea kweli akiwa Sociedad hata akafanikiwa kuzivutia timu nyingi barani Ulaya, msimu wake wa mwisho alifunga mabao 10 na kutoa asisti tatu kwenye mechi 40 za michuano yote.

MAISHA YAKE BINAFSI

Kwa kuijua asili yake Isaka amekuwa akitoa misaada mbali mbali kwenda nchini Eritrea kwa ajili ya kukuza vipaji na muda misaada ya kifedha na vyakula kwa watu wasiojiweza.

Licha ya pesa anazopata kupitia soka, jamaa sio mchezaji wa matanuzi, hamiliki magari yenye thamani kubwa kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengi.

Ni muda mchache utamuona kwenye maeneo ya starehe na akiwa hapo huwezi kuona akiwa anakunya pombe kali au vinywaji vyenye thamani.

Hii mwanetu ishikilie sana si kila mtu au mchezaji katika mafanikio yake lazima afanye mambo ya anasa eti kwa kuwa anapesa kama ilivyo kuwa tofauti kwa mchezaji huyu wa soka.

Kitu kingine nikukumbuka umetokea wapi na unatakiwa ufanye nini na kuna watu wangapi ulio waacha chini wanataka wakuone nini unafanya ambacho kitawakoa na wao kutoka katika hali Fulani walio kuwa nayo katika maisha kwasababu mafanikio ya mtu mmoja ni chanzo cha watu wengine kufanikiwa. Chukua hiyoooo mwanangu sanaaa!!!...






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post