Mtoto wa museveni atangaza nia ya urais 2026

Mtoto wa museveni atangaza nia ya urais 2026

Mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Jenerali wa Jeshi, kupitia ukurasa wake wa Twitter  amethibitisha kugombea kiti cha Urais wa Nchi huku akidai kuwa anajua Watu wengi walimtarajia kutangaza nia ya kugombea ifikapo 2026

Imeelezwa kuwa iwapo Muhoozi atagombea, atachuana na baba yake Rais Museveni aliyetangazwa kuwania Kiti hicho na Chama chake cha Resistance Movement (NRM) kwa muhula wa 7

Mnamo Januari 2023, Muhoozi  alidai kuwa ana uhakika wa kumrithi baba yake, Yower Museveni  ambaye ametawala nchi hiyo tokea mwaka 1986


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post