Mtoto wa Michael Jackson afichua siri, Sababu za kupuuza Birthday ya baba yake

Mtoto wa Michael Jackson afichua siri, Sababu za kupuuza Birthday ya baba yake

Mtoto wa muimbaji marehemu Michael Jackson, anayefahamika kama Paris Jackson amefichua sababu ya kuto-post picha ya baba yake kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

Jana ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa MJ ambapo kama angekuwa hai basi angekuwa anafikisha umri wa miaka 65, katika siku hiyo imekuwa tofauti na kuzua maswali kwa baadhi ya watu, kwani binti wa nyota huyo hakuonesha kusherekea kwa kum-post na kumtakia heri ya kuzaliwa baba yeke.

Kutokana na maneno hayo ambayo wengi walikua wakijiuliza, Paris amefichua na kuweka wazi kuwa hakumtakia heri ya kuzaliwa baba yake kwa sababu hata enzi za uhai wake MJ alikuwa haipendi siku hiyo na alichukia watu wanaosherekea siku ya kuzaliwa.

Paris akaenda mbali na kueleza kuwa ilifika wakati baba yake alikuwa akiwaficha siku yake ya kuzaliwa ili wasiadhimishe siku hiyo kwa namna yoyote, wakati akidai hayo binti huyo wa MJ alisema anaheshimu na kumpenda baba yake kwani ndiyo sababu ya yeye kuwepo.

Wakati akisema hayo akawahimiza mashabiki kutoa heshima kwa kufanya vitu ambavyo MJ alivipenda kama vile kuongeza ufahamu wa mabadiliko ya hali ya hewa, kufanya mambo kwa ajili ya mazingira, na harakati wa haki za utunzaji wa wanyama.

Binti huyo wa MJ sasa anafahamia kwa kipaji chake kikubwa cha kuimba na kuigiza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags