Mtoto wa Lil Durk adaiwa kumpiga risasa baba yake wa kambo

Mtoto wa Lil Durk adaiwa kumpiga risasa baba yake wa kambo

Mtoto wa kiume wa rapa kutoka nchini Marekani, #LilDurk, Romeo (10) anadaiwa kumpiga risasi baba yake wa kambo, kwa ajili ya kumtetea mama yake wakati wa mzozo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Post imeeleza hivi karibuni kamera za uchunguzi zimeonesha kuwa mtoto huyo alifyatua risasi na kumlenga baba yake mlezi aliyejulikana kama Joshua Pippens kwa ajili ya kumtetea mama yake, tukio lililotokea July 1,2024.

Aidha Joushua ambaye mpaka sasa yupo hospitali anapatiwa matibabu amedai kuwa mtoto wa Lil alichomoa bunduki kiunoni mwake kulingana na maagizo ya mama yake.

Hata hivyo mpaka sasa baba wa mtoto huyo mwenye watoto sita rapper Lil Durk (31) ambaye amewahi kufanya ngoma zikiwemo, All My Life, All love,  3 Headed Goat, Back Door, bado hajajibu chochote kuhusiana na tukio hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post