Mtoto wa Diddy ayakanyaga

Mtoto wa Diddy ayakanyaga

Mtoto wa mkali wa Hip-Hop kutoka nchini Marekani Diddy, King Combs anatarajiwa kufunguliwa mashitaka dhidi ya unyanyasaji wa kingono.

Kwa mujibu wa tovuti ya Vibe imeeleza kuwa mwanamke mmoja ambaye hajatambulika jina lake amepanga kumfungulia kesi King ya kumnyanyasa kingono pamoja na kumlazimisha kutumia dawa za kulevya.

Aidha kulingana na wakili anayewakilisha wanawake wote waliofungua kesi dhidi ya Diddy, Tyrone Blackburn ameweka wazi kuwa kesi hiyo iko mbioni kufunguliwa.

King Combs amewahi kuhusishwa kuwa kwenye mahusiano na wanawake tofauti tofauti akiwemo #BreaHick ambaye alidumu naye kwa miaka kadhaa na sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo #RavenTracy.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags