Mtoto atolewa Screw kwenye mapafu

Mtoto atolewa Screw kwenye mapafu

Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanikiwa kumtoa mtoto 'Skrubu' (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo alikua akiichezea mdomoni wakati akiwa shuleni na kwa bahati mbaya ikampalia.

Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Mwanaada Kilima amesema mtoto huyo alipaliwa na 'skurubu' hiyo siku nne zilizopita na kusababisha kukohoa sana.

Baba wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Msafiri Chatanda, amewashukuru watoa huduma na kuwaasa wazazi kuwakumbusha watoto madhara ya kuchezea vitu mdomoni.

Muhimbili wameripoti pia mwezi huu Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapato na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lilifanikiwa kuondoa shanga ya ‘plastiki’ iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Hata hivyo mapema jana, Daktari wa Magoniwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dk. Hedwiga Swai akishirikiana na wenzake walifanikiwa kumtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11 kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags