Mtanzania anayeigiza kama Sokwe alia na kejeli za watu

Mtanzania anayeigiza kama Sokwe alia na kejeli za watu

Hassan Michael maarufu kama ‘Hassan Gorila’ Mtanzania mwenye kipaji cha kuigiza miondoko ya Sokwe alia na baadhi ya watu kukejeli kipaji chake.

Amesema kati ya changamoto anazokumbana nazo ni kupata majeraha wakati wa kazi zake, pamoja na kupewa maoni ya kejeli kutoka kwa watu mbalimbali.

“Komenti nyingi ambazo naziona kwenye Instagram wanasema Afrika ni manyani na mimi nawaambia hapana hiyo ni sanaa ambayo naifanya kuna wengine wanasema nadhalilisha Afrika kutembea kama Sokwe, hizo ni kati ya changamoto ambazo nazipata kwa watu,” anasema.

Kutokana na vipaji hivyo Hassan ameeleza kuwa vimempatia mafanikio makubwa yakiwemo ya kupata mialiko kwenye nchi mbalimbali.

“Mafanikio niliyopata kutokana na vipaji vyangu ni kutembelea nchi za nje na kufanya ‘performance’ nimeenda Italia, Uturuki, Ujerumani, Australia, Bahrain pia napata mialiko mingi kutokana na sanaa yangu,” anasema.

Ikumbukwe kuwa siyo tu kutembea kama Sokwe Hassan anakipaji cha kutembea kama Kasa wa baharini, Nzi, Ngadu na Kenge.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags