Msigwa: Nimechoka kukaa na pesa za mama

Msigwa: Nimechoka kukaa na pesa za mama

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amedai kuwa amechoka kukaa na pesa za Mhe. Rais Samia Suluhu ambazo ametoa kama zawadi kwa ajili ya ‘klabu’ ya #Simba na #Yanga pindi wakishinda katika mashindano ya ‘klabu’ Bingwa Afrika.

Katibu huyo ameyasema hayo baada ya ‘timu’ hizo mbili siku ya jana kutoka bila ushindi ambapo jana ‘klabu’ ya #Yanga ilicheza na #Al ahly na kutoka sare, lakini pia kwa upande wa #Simba ambao walicheza dhidi ya ‘klabu’ ya #JwanengGalaxy  walitoka bila bila.

Msigwa ameeleza kuwa hapendi kurudi na pesa kila siku lakini anafahamu kuwa hayo ni mashindano hivyo amewapa moyo wachezaji wa ‘timu’ zote waongeze jitihada katika michezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags