Mshukiwa wa mauaji ya Tupac aomba kuachiwa huru

Mshukiwa wa mauaji ya Tupac aomba kuachiwa huru

Mshukiwa wa mauaji ya ‘rapa’ kutoka Marekani Tupac Shakur, Duane “Keefe D” Davis, amewasilisha ombi la kuachiwa huru kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani aliyokuwa nao kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa maelezo yake mahakamani siku ya jumanne June 25, Keefe D alieleza kuwa ugonjwa wake wa saratani umefika katika level mbaya kutokana na kukosa vyakula vyenye vitamini.

“Nina saratani ya utumbo mpana kwa muda mrefu sana, nimekuwa gerezani nikila vyakula vilivyosindikwa, viazi bandia, maziwa bandia kila kitu cha bandia na wala hawatoi matunda hali hii sio nzuri kwa mgonjwa wa saratani, niko katika hali mbaya na nitafanya chochote kuokoa maisha yangu”

Ili kufanikishwa kuachiwa huru meneja wa muziki nchini humo anaye wasimamia wasanii Blueface na The Game aitwaye Wack 100 alimtolea dhamana ya dola 750,000 Keefe D lakini hakimu alikataa kumwachilia huru.

Davis Keefe D mwenye umri wa miaka 60 amekuwa kizuizini tangu akamatwe Septemba 29, 2023 wakati akiwa anafanya mazoezi karibu na nyumbani kwake jijini Las Vegas.

Ikumbukwe kuwa Tupac alizaliwa Juni 16, 1971 na alifariki September 13, 1996 akiwa na miaka 25, huku kesi ya mauaji ya kifo chake bado inaendelea mahakamani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags