Mshukiwa Mauaji Ya Tupac Azichapa Gerezani

Mshukiwa Mauaji Ya Tupac Azichapa Gerezani

Mshukiwa wa mauaji ya mkali wa Hip Hop Marekani Tupac, Duane “Keefe D” Davis, ameripotiwa kuzichapa gerezani na mfungwa mwenzake katika gereza lililopo Kaunti ya Clark jijini Las Vegas.

Kufuatia ripoti iliyotolewa na maafisa wameeleza kuwa mapigano hayo yalikuwa ya nguvu na kuwafanya waingilie kati wakitumia maji ya kuwasha kuwatenganisha wafungwa hao.

Kutokana na tukio hilo, Davis sasa anakabiliwa na shtaka la ziada la shambulio na mfungwa mwenzake, kulingana na nyaraka za kisheria zilizopatikana na tovuti ya TMZ zinaeleza kuwa Davis aliwaambia maafisa kuwa alikuwa akijitetea.

Davis amekuwa gerezani tangu Septemba 2023, na kufunguliwa mashtaka ya madai ya kuhusiaka katika mauaji ya msanii Tupac Shakur mwaka 1996. Davis amekana shtaka hilo la mauaji, na kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa Machi 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags