Mrembo anayekula toilet paper

Mrembo anayekula toilet paper

Kila mtu huwa na uraibu wake ambao kwa upande wake huona ni sawa lakini kwa watu wengine huutazama uraibu huo kama kitu cha ajabu, kuna wale wanaopenda kula, kucha, udongo na mara nyingi kila waendapo utawakuta wamehifadhi udongo sehemu kwaajili ya kula.

Ukiachana na hao wala udongo ambao kila siku unawaona , fahamu kuwa wapo wanaokula vitu vya ajabu zaidi kuliko udongo, kama afanyavyo mrembo  anayefahamika kwa jina la Kinah, kutoka nchini Marekani ambaye yeye hula karatasi za chooni (Toilet Paper) muda wote.

Kwa mujibu wa #Interview aliyofanya mrembo huyo na  TLC Network , ameeleza kuwa anapendelea kula karatasi hizo siku nzima, mara baada tu ya kuamka huzifanya chakula chake wakati mwingine hata kabla ya kusafisha kinywa chake na popote anapoenda ikiwa ni pamoja na kazini, kwenye gari, nyumbani na wakati mwingine hata akiwa saloon hutumia karatasi hizo kama chakula.

Tabia hiyo ya kula karatasi za chooni ameanza miaka 20 nyuma iliyopita, anaeleza kuwa kwa siku hujikuta akitumia hadi bunda 4 za karatasi hizo, na kila mwaka hujikuta akiingia gharama ya dola 2,700 ambayo ni zaidi ya milioni Tsh 6.

Katika mahojiano yake hayo ameeleza kuwa haoni ubaya wowote kwake yeye kula karatasi hizo, kwani huzitumia kama ambavyo mtu yeyote anavyokula kitu akipendacho , huku akiendelea kudai kuwa huwa haoni shida yoyote katika kula karatasi hizo japo watu wengi humuona kama mtu wa ajabu na mara nyingi wakimuona anakula karatasi hizo basi huanza kumpika picha na wengine kumchukua video.

Tuambie uraibu wako wewe ni nini?

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags