Mr. Flavour aungana na Burna Boy, Diamond

Mr. Flavour aungana na Burna Boy, Diamond

Na Asma Hamis

Msanii wa Nigeria na mmiliki wa label ya ‘2nite Entertainment’ Mr. Flavour ameungana na wasanii wengine kama Diamond na Burna baada ya kusaini mkataba na kampuni ya muziki ya Warner Music Africa na Africori.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Music in Africa’ inaelezea kuwa mkataba huu utamruhusu Flavour kutumia mtandao wa Warner Music kusambaza muziki wake kimataifa huku akitumia timu ya masoko ya A&R.

“Nina furaha na shauku kubwa kufanya kazi na Warner Music pamoja na Africori katika awamu hii mpya ya kazi yangu, ni muhimu kwangu kushirikiana na kampuni inayounga mkono ubunifu wa kazi yangu ya kisanii,” amesema Flavour

Hata hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Warner Music Africa, Temi Adeniji ameeleza kuwa kufanya kazi na Flavour kutaimarisha tasnia ya muziki Afrika.

“Kushirikiana na Flavour ni hatua kubwa katika mipango yetu ya ukuaji na maendeleo hii inaonyesha dhamira yetu ya kuwawezesha wasanii wa kiwango cha kimataifa, wasanii kama Flavour ndio watakaoendelea kuunda mustakabali wa tasnia ya muziki wa Afrika.” amesema Temi Adeniji

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Africori, Yoel Kenan aliongeza kwa kueleza “Tunamkaribisha Flavour kwenye timu nguvu zake, ubunifu wake, na sauti yake ya kipekee ni mfano wa mvuto wa muziki wa Kiafrika leo, tunatazamia kufanya kazi pamoja katika hatua hii mpya ya kazi yake, kuendelea kukuza hadhira yake na kusambaza sauti yake sehemu mpya,”

Aidha mbali na Mr Flavour wasanii wengine kutoka Afrika ambao wameshamwaga wino katuka kampuni hiyo ni pamoja na Diamond Platnumz, Burna Boy, Joe Boy, Ckay na wengineo wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags