Mr Ibu kuzikwa leo

Mr Ibu kuzikwa leo

Marehemu mwigizaji kutoka nchini #Nigeria John Okafor (62) maarufu Mr Ibu anatarajia kuzikwa leo Juni 28, 2024 katika mji aliozaliwa wa #Amuri, Jimbo la #Enugu.

Mr Ibu alifariki dunia Machi 2, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Evercare iliyopo nchini Nigeria.

Kufuatia na video inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwaonesha wadau mbalimbali wakijumuika katika mazishi ya mwigizaji huyo huku akitarajiwa kupumzishwa katika makazi yake ya milele jioni ya leo.

Taarifa ya mazishi hayo kufanyika leo ilitolewa na kaka mkubwa wa Mr Ibu, Sunday Okafor, ambapo alieleza kuwa waliamua kuchelewesha mazishi hayo kwa ajili ya kumpatia mazishi ya kihistoria mwigizaji huyo.

Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia filamu zake kama The Collaborator, My Chop Money na nyingine nyingi akiwa na #Aki na #Ukwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags