Mr Blue: Muda wa kuwaletea kazi

Mr Blue: Muda wa kuwaletea kazi

Mwanamuziki wa Hip-hop nchini Mr Blue ameweka wazi kuwa umefika muda wa kuachia kazi mfululizo kwa mashabiki wake, huku akiwataka wachague aina gani muziki aanze nao kati ya hip-hop, Bongofleva au Amapiano.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr Blue ameweka wazi kuwa anakazi za kutosha ambazo yupo tayari kuzitoa hivyo mashabiki wachague aanze kutoa kigongo kipi.
Mapema 2024 Mr Blue alirudi masikioni mwa mashabiki kwenye wimbo wake wa ‘Mapozi’ uliofanyiwa remix na Diamond.

Aidha remix hiyo ambayo pia alishirikishwa Jay Melody iliachiwa rasmi miezi minne iliyopita na hadi kufikia sasa imefikisha watazamaji 4.5 milioni, kwenye mtandao wa YouTube.

Utakumbuka kuwa mkali huyo wa hip-hop amewahi kutamba na ngoma zake kama ‘Mama la Mama’, ‘Baki na Mimi’, ‘Mbwa Koko’ na nyinginezo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post