Mr Blue atangaza kufungua studio

Mr Blue atangaza kufungua studio

Baada ya kutoa taarifa kuwa anakuja na ngoma mfululizo kupitia ukurasa wake wa Instagram na sasa ‘rapa’ Mr Blue ametangaza kufungua studio yake ya muziki iliyoipa jina la ‘Blue Records’.

Mr Blue amelithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa ku-share Logo inayotambulisha studio yake hiyo huku akiweka wazi kuwa yamebaki masaa machache ya kutoa kazi mpya.

Mr Blue alirudi tena masikioni mwa mashabiki kwa mara nyingine mapema 2024 kwenye wimbo wake wa ‘Mapozi’ uliofanyiwa remix na Diamond.

Aidha remix hiyo ambayo pia alishirikishwa Jay Melody iliachiwa rasmi miezi minne iliyopita na hadi kufikia sasa imefikisha watazamaji 4.5 milioni, kwenye mtandao wa YouTube.

Utakumbuka kuwa mkali huyo wa hip-hop amewahi kutamba na ngoma zake kama ‘Mama la Mama’, ‘Baki na Mimi’, ‘Mbwa Koko’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags