Mtengeneza maudhui kutoka nchini Marekani Mr Beast ambaye alijulikana zaidi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuzikwa akiwa hai kwa siku saba, ameripotiwa kuwekeza mpunga mrefu kwa ajili ya shindao alilolipa jina la ‘Beast Games’.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali Marekani Mr Beast ameungana na mtandao wa Amazoni kuwekeza dola milioni 14 kujengea mji jijini Toronto kwa ajili ya shindano hilo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa ‘Amazon Prime Video’ Desemba 19, 2024.
Aidha mashindao hayo yameripotiwa kuhusisha washiriki 1,000 huku mshindi akiondoka na dola milioni 5 ambapo shindano hilo linatajwa kuwa la kihistoria kwani linatarajiwa kutazamwa na watu wengi siku hiyo.
Ikuimbukwe kuwa mtengeneza maudhui huyo alipata umaarufu zaidi na kuishangaza dunia baada ya kuvunja rekodi ya kuzikwa na kutoka akiwa hai ndani ya siku saba tukio lililotokea Novemba 2023.
Mr Beast mwenye umri wa miaka 26 alitengeneza jeneza lenye mfumo wa umeme ambalo pia lina mfumo wa hewa, kamera, chakula na maji.
Hata hivyo, katika siku saba ambazo Mr Beast ‘alizikwa hai’ aliendelea kuwasiliana na rafiki zake ambao waliweka kambi juu ya kaburi lake huku wakifuatilia usalama na afya yake.
Leave a Reply