Na Michael Anderson
Mambo vipi pande za vyuoni? tunapoanza mwaka mpya wa masomo tambua kwamba unahitaji kuongeza thamani zaidi katika maisha yako binafsi ikiwa unasogea kuingia kitaa.
Leo nitazungumzia wapambanaji wote wa vyuoni wafanyabiashara wadogo ,watu wenye vipaji , na wanaopambana kwa ajili ya wengine.
Neno mafanikio kila mtu huwa na maana yake kwa wakati wake na kwa eneo lake katika maisha.
Kuna mafanikio ya kiafya, kiuchumi, kifedha na hata yale ya uhusiano mzuri nk. Yote hayo na mengine mengi ni sehemu mojawapo ya maeneo ambayo kila mtu huhitaji kufanikiwa .
FANYA HAYA UFANIKIWE KATIKA MAPAMBANO YAKO
1.IMANI NA IBADA
Pasipo Mungu hakuna maisha hivyo zingatia sana kumuomba yeye kwa kila hatua ya maisha yako kutokana na imani yako.
2.KUFANYA KAZI KWA BIDII
Suala zima la kufanikiwa katika maisha linahitaji kujitoa na kujikana kila mara iitwapo leo ili kuhakikisha unafanikiwa na kuwa na mwelekeo mzuri na mwema wa kimaisha.
Kufanya kazi kwa bidii huendana na ufanisi na ujuzi ulionao, ambapo katika vyote hivyo ukizingatia vitaleta matokeo chanya na tofauti katika ulimwengu wako wa mafanikio.
Acha kuwa mtu wa malalamiko na kukata tamaa haraka, anza kuanzia sasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato chako cha kila siku unachohitaji maishani.
3.Uhusiano mzuri na watu.
Katika dunia ya leo kama unahitaji kufikia mafanikio makubwa zaidi maishani mwako, hili ndio jambo au siri muhimu unayopaswa kuitekeleza haraka na kuizingatia kwa umakini mkubwa.
Kuwa na uhusiano mzuri na watu wa karibu yako ni jambo jema linaloweza kukuweka katika mazingira mazuri zaidi ya mafanikio ukawa mtu wa tofauti katika nyanja zote za kimaisha.
Kama ukikosa uhusiano mzuri na watu kuna athari kubwa ya kukosa furaha na amani kama ukikosa furaha na amani kuna athari kubwa pia ya kukosa uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na bidii.
4.Kuwa na nidhamu
Hili ni jambo ambalo watu wengi wa jamii zetu tunaona wameshindwa kulifanikisha kwa asilimia kubwa katika mazingira yao ya kimaisha na kazi, hivyo limesababisha watu wengi kushindwa kufikia malengo makubwa na mazuri waliojiwekea maishani mwao.
5.Nidhamu ya fedha.
Suala la kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha limenenwa sana na watu wengi katika dunia ya leo. Waandishi wengi wa vitabu vya kibiashara na maendeleo ya mtu binafsi wamejaribu kulisema na kulielezea jambo hili kwa ufanisi katika vitabu vyao mbalimbali walivyovitoa.
6.Kujiamini na kujikubali binafsi
Ni moja ya siri kubwa ambayo watu wengi hawajaitambua. Kujiamini ni hali pekee ndani ya mtu ya kuwa jasiri bila uogo katika jambo lolote lile analolikabili mbele yake. Huku kujikubali pia ni sehemu muhimu inayomfanya mtu kujiona tofauti na wa kipekee katika mazingira ya kile anachokifanya au kutaka kukifanya
Leave a Reply