Motsepe: goli la Aziz Ki lilikuwa ni halali

Motsepe: goli la Aziz Ki lilikuwa ni halali

Rais wa shirikisho la 'soka' Afrika (CAF), Patrice Motsepe amekiri kuwa goli la #Yanga lililokataliwa na mwamuzi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mamelod Sundowns Afrika Kusini lililofungwa na Aziz Ki lilikuwa goli halali.

Rais Motsepe ameyasema hayo leo alipowasili visiwani #Zanzibar katika fainali za ‘African schools football’ na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa #TFF Wallace Karia.

“Nafahamu Rais wa CAF hapaswi kutoa maoni ila nikitazama kama Shabiki wa mpira ile mechi ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns lile kwa mtazamo ni bao halali kabisa Yanga walifunga, tukisema tuongee mpira bila kutazama Urais wa #CAF lile ni goli halali Yanga walistahili” amesema #Motsepe

Mchezo huo kati ya Mabingwa wa ligi kuu ya #NBC Yanga, dhidi ya #Mamelod mzunguko wa kwanza ulichezwa Machi 30, 2024, na kuja kurudiwa Afrika Kusini April 5, mwaka huu huku Yanga ikiondolewa kwa mikwaju ya penati 3-2.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post