Moto wazidi kumuwakia Sancho, Aondolewa kwenye group

Moto wazidi kumuwakia Sancho, Aondolewa kwenye group

Winga wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, #JadonSancho kwa upande wake mambo yanazidi kuwa makubwa kila kukicha huku muafaka baina yake na ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo  Erik Ten Hag ukionekana kukosekana kabisa.

Inadaiwa kuwa #Sancho ameondolewa kwenye Group la WhatsApp la #ManchesterUnited ambalo ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo hulitumia kufikisha taarifa muhimu kwa wachezaji wake.

Matatizo ya Sancho huko #OldTrafford yalianza tangu mwezi Septemba alipomshutumu #TenHag kwa uongo juu ya sababu ya kuachwa kwenye kikosi cha #ManUnited kilichopigwa mabao 3-1 na Arsenal.

 Kutokana mgogoro huo mchezaji huyo aliondolewa katika uchaguzi wa kikosi cha kwanza lakini pia kwenye uwanja wa mazoezi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags