Moni: Mwakani Hakuna Msanii Atagusa Moto wa Moco

Moni: Mwakani Hakuna Msanii Atagusa Moto wa Moco

Rapa Malume Centrozone ameendelea kuwatambia rapa wenzake kutokana na mapokezi ambayo amekuwa akipata kila apandapo jukwaani na Country Wizzy ambaye wanaunda kundi la Moco.

Mapema leo Moni ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa mwakani mashabiki watarajie kazi nyingi kutoka kwake na Country na hakuna msanii atayeweza kuuzima moto wao.

"Mwaka Jana Mlinipa Sana Hasira Mwaka Huu Tumejenga Zege Mungu Akijaalia Mwakani Inshaalah Hakuna Msanii Atagusa Moto Wa (MOCO) Moni Centrozone & Country Wizzy I PROMISE YOU THAT," ameandika Moni.

Hata hivyo Malume ameonesha ukomavu wake hata baada ya kushushiwa video ya wimbo wa Maelekezo Chapter 3 kwenye mtandao wa YouTube na kuibiwa akaunti yake ya Instagram mwaka jana, ambayo ilikuwa na wafuasi wengi.

"Matter Of Fact Hivi Ndo Inatakiwa Ufanye Ukikutana Na Changamoto This Is How You Came Back Baada ya Kupoteza Social Media Na Kushushiwa Mangoma Hovyo YouTube," ameandika Malume

Moco ni moja kati ya combo ya Moni & Country Wizzy ambao walianza kufanya kazi pamoja rasmi 2018 na wameshatoa ngoma zilizofanya poa kama vile Mwaa, Toto na zingine nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags