Modric awasikitisha mashabiki

Modric awasikitisha mashabiki

Mashabiki wa ‘soka’ wamedai kiungo wa #RealMadrid #LukaModric ametumia nguvu nyingi kuzuia kumwaga machozi baada ya Croatia kugomewa ushindi katika mchezo ambao makali yake ya uwanjani yamemfanya achaguliwe kuwa mchezaji bora wa mechi.

Kiungo huyo veterani alionyesha kiwango bora, lakini hilo halikutosha kuipa ushindi timu yake na hivyo kupata sare ya 1-1 na Italia katika mchezo wa mwisho wa makundi wa fainali za Euro 2024.

Modric aliifungia Croatia bao la kuongoza kwenye dakika 55 ikiwa ni dakika chache baada ya kukosa penalti.

Ushindi ungewapa Croatia nafasi ya kutinga kwenye hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo, lakini sasa imebaki kwenye nafasi ya tatu kwenye kundi lake, ikisubiri matokeo ya makundi mengine ili kufahamu hatima yao kama watasonga mbele au la.

Italia ili ilisawazisha dakika 98 kupitia kwa mtokea benchini Mattia Zaccagni. Matokeo hayo yalifanya Italia kushika nafasi ya pili, huku Hispania ikiongoza kundi hilo na Croatia kwenye nafasi ya tatu na pointi zao mbili ilizovuna kwenye mechi tatu.

Mashabiki walihuzunishwa na uso wa Modric wakati anahojiwa mwishoni mwa mechi hiyo na shabiki mmoja alisema: “Alionekana kama ametoka kulia, pole sana Modric.”

Mwingine alisema: “Huruma sana kumaliza mambo kwa namna ile.” Na shabiki wa tatu alisema: “Maumivu yamejionyesha wazi usoni. Aliumizwa sana kwa bao lile la dakika za mwisho.” Na shabiki mwingine aliongeza: “Hakustahili matokeo haya, inauma sana.”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags