Mnaosoma meseji zetu kwenye daladala hamuoni aibu

Mnaosoma meseji zetu kwenye daladala hamuoni aibu

Binadamu hawaishiwi vioja, starehe ni nyingi duniani lakini wapo ambao wamechagua kupiga chabo mambo yasiyowahusu.

Achana na wale wa madirishani, au wazee wakuiga hadi jina kwenye chumba cha mtihani, wapo hawa niyu modeli kwenye daladala, ambao wao kupitishwa kituo siyo ajabu, kikubwa wajue mwisho stori itaishiaje.

Kumekuwa na kijitabia f'laani hivi kwenye daladala kumkuta mwamba aliyesimama kwa kukosa siti akipiga chapo kwenye meseji za mtu aliyekaa.

Tena bila ya aibu kama meseji zinachekesha utamuona na yeye anakenua meno,shida inabaki kwa msomewaji meseji kutafuta mbinu ya kuficha mawasiliano yake.

Juzi kati wakati naenda kitaani kwetu uvumilivu ukanishinda kwenye daladala nikaamua nikapunguza mwanga na saizi ya maneno baada ya kugundua jamaa anapiga chabo. Cha ajabu na yeye akashindwa kuvumilia akaropoka "ongeza mwanga tusome wote".






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags