Mmoja apona ugonjwa wa Marburg

Mmoja apona ugonjwa wa Marburg

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia leo tarehe 4 April 2023, jumla ya waliougua ugonjwa wa Marburg Wilaya ya Bukoba vijijini, Kagera ni nane na kati yao watano wamefariki.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, amesema kuwa “Ni jambo la kumshukuru wwenyezi mungu kuwa hatujapata wagonjwa wapya wala vifo, aidha ninayo furaha kubwa kuwajulisha kuwa leo tumemruhusu Mgonjwa mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 26 akiwa na afya njema, ni matumaini yangu kuwa jamii itampokea vyema na kushirikiana nae katika shughuli zake za kila siku” amesema Ummy

Aidha aliendelea kuelezaea kuhusu waliochangamana na wagonjwa na kueleza kuwa“Hadi kufikia leo watu 212 waliotangamana na wagonjwa wamebainishwa, kati ya hawa watu 35 wamemaliza siku 21 za uangalizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa huu na hivyo tumewaruhusu kutoka katika karantini na kurejea kwenye Familia na shughuli zao” amesema Ummy Mwalimu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags