Mmiliki wa ndege ya precision Air afariki dunia

Mmiliki wa ndege ya precision Air afariki dunia

Mmiliki na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege ya Precision Air, Michael Ngaleku Shirima amefariki dunia jana saa tatu usiku Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu tangu juzi June 8. 

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo ya ndege ya Precision Air leo asubuhi imethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema taarifa zaidi za mazishi ya Mzee Shirima aliyefariki akiwa na umri wa miaka 80 zitatolewa na familia yake.

Aidha kwa mujibu wa wikipedia, Mzee Michael Ngaleku Shirima alianzisha Shirika hilo la Ndege miaka thelathini iliyopita (1993) Arusha akiwa na Ndege ya Abiria watano ya Piper Aztec akisafirisha Watalii kwenda Mbuga za wanyama kama Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar. 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags