Mkopo wamtokea puani Chris Brown

Mkopo wamtokea puani Chris Brown


Baada ya kukopa mkopo kwa ajili ya kununulia migahawa miwili ya Popeyes Chicken na kushindwa kulipa deni, sasa mwanamuziki Chris Brown ametakiwa kulipa deni hilo na mahakama jijini Los Angeles.

Brown anatakiwa kulipa kiasi cha dola 1.7 milioni ambayo ni zaidi ya tsh 4.3 bilioni alizokopo katika benki ya City National.

Aidha brown amepewa siku 30 kukamilisha taratibu za kulipa deni hilo na endapo akishindwa huenda mali zilizopo nyumbani kwake zikachukuliwa na kupigwa mnada ili benki iweze kurejesha pesa yao.

Ikumbukwe kuwa kesi ya madai dhidi ya Brown ilifunguliwa Sep 2023, baada ya msanii huyo kushindwa kulipa mkopo. Hata hivyo licha ya kushindwa kulipa deni hilo hata ununuzi wa migahawa hiyo pia haukufanikiwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags