Mke wa Alikiba adai talaka yake

Mke wa Alikiba adai talaka yake

Mwanadada Amina Khalef ambae ni mke wa Alikiba, amevinja ukimya na kudai kuchoshwa na tabia za kuvunjiwa heshima hadharani ambazo anatendewa na mumewe.

kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanadada huyo alifunguka mazito kwa kuweka wazi hisia zake kupitia insta story ambapo amesema;



“Nimeona kuna haja ya kulizungumza, nafikiri hii imezidi. Nimechoshwa kuvunjiwa heshima hadharani huku watu wakiwa hawaelewi hali iliyopo katika kivuli cha mke wa mtu" alieendelea kwa kusema

“Nimeondoka kwenye maisha yako kuepuka maumivu, unyanyasaji na mengine mengi lakini mpaka leo hutaki kunipatia Talaka huku wewe (Alikiba) ukiwa huru kufanya mambo yako na mimi ukinifunga katika kivuli cha mke wa mtu" akamalizia kwa kuandika

“Kimsingi naomba usaini karatasi ili nipate Talaka kila mmoja aendelee kuwa huru” ameandika Amina mke wa Alikiba

Ikumbukwe tuu ndoa hiyo ya King Kiba na Amina ilifungwa mwezi Aprili, 2018 na kubahatika kupata watoto wawili, Keyaan Kiba na Kamran Kiba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags