Mkali wa Black Panther afariki na watoto wake watatu

Mkali wa Black Panther afariki na watoto wake watatu

Muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani, Taraja Ramsess amefariki dunia akiwa na watoto wake watatu baada ya gari lake kugonga trekta.

Taraja ambaye ameonekana katika movie ya Black Panther alifariki baada ya gari lao kugonga trekta lililokuwa limeharibika katikati ya barabara katika kaunti ya Dekalb, Georgia usiku wa Halloween ambapo alikuwa na watoto wake 5.

Taarifa hiyo, imetolewa rasmi na familia ya muigizaji huyo kwa kueleza kuwa watoto hao watatu ambao ni  Sundari (13), Fuginop (10)  na mwingine wa wiki nane wote wamefariki na baba yao katika ajali hiyo huku watoto wawili wakiwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu.

Ikumbukwe kuwa mwamba huyo alionekana katika filamu mbalimbali ikiwemo Black Panther, Avengers, Avengers: Infinity War na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags