Mjengo wa mwigizaji Cara wateketea kwa moto

Mjengo wa mwigizaji Cara wateketea kwa moto

Jumba la kifahari la mwanamitindo na mwigizaji kutoka nchini Marekani Cara Delevingne (31) lateketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, huku watu wawili wakijeruhiwa akiwemo askali wa zima moto.

Kufuatiwa na ripoti hiyo imeelezwa kuwa mwigizaji huyo hakuwepo nyumbani kwa wakati tukio hilo linatokea ambapo chanzo cha moto huo kikitajwa kuwa ni shoti ya umeme.

Baada ya kumalizika kwa uokoaji na kuzima moto huo Cara ali-share picha za paka wake wawili ambao waliokolewa katika ajali hiyo ikiambatana na ujumbe wa shukrani kwa zimamoto na watu waliojitokeza kusaidia

“Moyo wangu umevunjika leo. Siwezi kuamini. Maisha yanaweza kubadilika kwa kufumba na kufumbua. Hivyo thamini ulichonacho, asanteni sana zimamoto na wote mliojitokeza kuja kusaidia”

Cara Delevingne ameonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘Valerian and the City of a Thousand Planets’, ‘Suicide Squad’, ‘Life in a Year’, ‘Paper Towns’ ‘Tell It Like a Woman’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags