Mitindo mizuri ya nywele ya kwendea kazini

Mitindo mizuri ya nywele ya kwendea kazini

Na Glorian Sulle

Moja ya tatizo ambalo limekuwa likiwachanganya wengi haswa mabinti ni muonekano wa kichwani, yaani atatokelezea vipi akienda kazini wiki nzima.

Kutokana na hilo Mwananchi Scoop imekuletea aina ya nywele ambazo zitakufanya uwe na muonekano mzuri wakati wote uwapo kazini.

Kubana nywele zako

Kama umesuka nywele ndefu mfano mabutu ya rasta na nyinginezo pendelea zaidi kubana nyuma au juu (kidoti) hii itapunguza usumbufu wa nywele unapokua katika utendaji wako wa kazi, hasa unapoongea na mgeni, mteja au boss wako kubana kutakupa kujiamini zaidi.

Unapoachia nywele mpaka usoni itakuletea usumbufu wa kuziweka sawa kila mara, hii unaweza kuona ni sawa ukiwa pekeyako lakini ukiwa na mtu anayekusikiliza au unayemuhudumia itapunguza umakini wake.

Chagua nywele zenye urefu wa kawaida

Kama ilivyo kawaida ya mabinti wengi kupenda kusuka nywele ndefu wanapokua kazini, pia wanatakiwa kufahamu kuwa nywele hizo kwenye ofisi official si mahali pake, hivyo wanatakiwa kusuka nywele za kawaida zitakazowapa muonekano mzuri, chakuzingatia ni kujua kila nywele ina mahala pake.

Jaribu kuwaza upo kazini tena kwenye kikao na boss na wafanyakazi wenzako halafu unatakiwa kunyanyuka na kuelezea kitu, gafla umenyanyuka nywele imevutwa na kiti unaanza kuitoa ndiyo uende mbele, je bado utakua na ujasiri uleule?

Hivyo basi nywele za wastani uwapo kazini ni muhimu sana kuliko kusuka nywele ndefu .

Chagua nywele zenye rangi ya kawaida

Kumekua na baadhi ya swaga kwa watu kusuka nywele za rangi mbalimbali, ni sawa kusuka lakini si za kwendea kazini kuna rangi za nywele hazileti picha nzuri ofisini embu fikiria unakwenda ofisi yenye heshima ukiwa umesuka nywele za rangi ya njano au blue, lazima watu wakufikirie tofauti.

Hivyo basi ili uweze kudamshi inabidi uangalie rangi ya nywele ambayo haitamkwaza mtu.

Kwa wale wanaovaa mawigi, vaa wigi fupi

Kazini ni sehemu official hivyo kuna aina ya mionekano haipaswi uwe nayo kama tunavyojua kitambulisho kikubwa cha binadamu ni kichwa hivyo basi zingatia sana kuanzia kwenye nywele hadi kwenye shingo utambulisho wako ukae mahala pake.

Blichi

Moja kati ya mitindo ambayo imeingia  mtaani kwa siku za hivi karibuni ni baadhi ya wadada kunyoa na kuweka blichi, sasa hapa turekebishane kidogo hukatazwi kufanya hivyo bali unapoweka blichi unatakiwa kuangalia kama ulichokiweka kichwani kinaendana na rangi yako ili kuepusha kunyooshewa vidole na kuchekwa.

Endapo utaamua kuweka blichi basi chagua rangi ambayo unaweza kuingia nayo sehemu yoyote,  epuka kupaka rangi zenye mng’ao sana unaweza kukutana na kiongozi ukashidnwa hata kupata picha naye ya pamoja kutokana na muonekano huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudokaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post