Mike Tyson kurudi tena ulingoni

Mike Tyson kurudi tena ulingoni

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Marekani Mike Tyson (58) atarajia kurudi tena ulingoni Julai 20 mwaka huu akizichapa na Jake Paul (27), pambano ambalo litafanyika katika uwanja wa AT&T uliopo jijini Texas pia litaoneshwa live kupitia mtandao wa Netflix.

Kufuatiwa na pambano hilo wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi wamekuwa na wasiwasi huenda bondia huyo akapigwa kutokana na umri wake pamoja na kutokufanya mazoezi kwa muda mrefu.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Tyson ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa juu aliingia ulingoni mwaka 2020, ambapo lilikuwa ni pambano la raundi nane dhidi ya Roy Jones Jr huko Los Angeles.

Aidha kwa upande wa Jake Paul amekuwa na mafanikio kadhaa katika mchezo huo ambapo katika rekodi yake ameshawahi kuwashinda nyota wa zamani wa UFC kama Nate Diaz, Anderson Silva, Tyron Woodley, Andre August na Bourland.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags