Miaka miwili ya ndoa, Billnass ajivunia mtoto

Miaka miwili ya ndoa, Billnass ajivunia mtoto


Mwanamuziki Billnass ameeleza kuwa katika miaka miwili ya ndoa yake na Nandy, kuna vingi anajivunia lakini kikubwa ni kupata mtoto wa kike.

"Tunashukuru Mungu kwa kila jema alilotujaalia hadi muda huu, pumzi ya uhai ndiyo kitu kikubwa kuliko vyote, na leo nina furaha kubwa na kujivunia kutimiza miaka miwili kwenye ndoa na mke wangu Faustina Mfinanga 'Nandy', kubwa zaidi ya mafanikio ni kujivunia pia kupata mtoto wa kike ninayempenda sana," amesema

Hata hivyo ameongezea kuwa katika miaka hiyo miwili ya ndoa yao ataendelea kumpenda Nandy katika maisha yake yote

"Ni safari ndefu isiyokuwa na kikomo, hii kumbukumbu ya ndoa yetu mke wangu upendo na uvumilivu alionionesha kwa kipindi hiki chote sina cha kusema zaidi ya shukrani, Mungu atubariki sisi na familia yetu. Nampenda zaidi na nitaendelea kumpenda na kumjali hadi mwisho wa maisha yangu duniani kwani najijua mimi ni zaidi ya pasua kichwa ila milima na mabonde, vizingiti na mito, maziwa bahari kwa uwezo wake Mungu tu tutavuka," amesema.

Utakumbuka kuwa William Lyimo 'Billnass' na nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga 'Nandy' wametimiza miaka miwili ya ndoa yao tangu walipofunga, Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Aidha katika kuonesha furaha ya siku hiyo kupitia mtandao wa Instagram Nandy alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram uliokuwa na maneno yaliyoonesha furaha yake kutumiza miaka hiyo

"Mume wangu, miaka miwili ya ndoa yetu imekuwa fundisho kubwa kwangu kujua upendo ni kitu muhimu sana, uwepo wako umerahisisha maisha yangu na ya kipenzi chako NAYA, jua tu tunakupenda sana.

"Ninachokuomba, najua wanaume mmeumbiwa kupepesa macho japo sio mwanamume wangu wewe (joke) popote uendapo, chochote ufanyacho jua una watu wanakupenda na kukuhitaji sana,kuyashinda majaribu 'now days' ni rahisi sababu kila kitu kishapitwa na wakati na wakati wenyewe ndo sasa kuonyesha mfano na kuwa mifano bora kwa watu wenye mapenzi ya kweli, kuwa vijana wakiamua inawezekana",ameandika Nandy






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags