Miaka 31 ya Zuchu na karata mbili kubwa

Miaka 31 ya Zuchu na karata mbili kubwa

Ikiwa leo ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Zuchu akitimiza miaka 31 yapo mengi ambayo yamemgusa katika tasnia yake, lakini kwa kawaida mambo haya mawili tunaweza kuseme katika miaka yake hiyo ndio mambo aliyokuwa akiyaota.

Zuchu kuingia Usafini
Kulikuwa na maswali mengi haswa katika mitandao ya kijamii ni msanii gani ambaye anakwenda kutoana jasho na Queen Darling Usafini.

Na hatimaye Aprili 2020 zali la mentali lilimuangukia mtoto kutoka katika visiwa vya karafuu Zanzibar ambaye pia ni binti wa mwimbaji wa taarabu malkia Khadija Kopa, Zuhura Othman ‘Zuchu’ akitoka na EP ya vibao saba iliyopewa jina la ‘I am Zuchu’ iliyotawaliwa na ngoma kama Hakuna Kulala, Wana’, Raha na nyinginezo.

Ngoma ya Sukari kuweka rekodi Afrika Mashariki
Jambo jingine la pili kubwa ambalo liligusa tasnia yake moja kwa moja ni kufikia rekodi ya mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Yemi Alade kupitia wimbo wa ‘Sukari’ kufikisha zaidi ya wasikilizaji milioni 300 katika mtandao wa Boomplay huku kwenye mtandao wenye ushawishi mkubwa YouTube wimbo huo ukitazamwa zaidi ya mara milioni 100






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags