Miaka 3 jela kwa kupokea rushwa

Miaka 3 jela kwa kupokea rushwa

Manaume mmoja aliefahamika kwa jila la Magesa Ngereja amekutwa na hatia ya kupokea hongo kwa lengo la kuuza ardhi ya kijiji cha Kahangaza, kitongoji cha Kanyamlima mkoani Kagera.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Muleba mkoani humo dhidi  ya mashtaka hayo.

Mshtakiwa alikutwa na kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa sura ya 329 mapitio ya 2022 baada mahakama kujiridhisha kwa kusikiliza ushahidi wa pande zote.

Aidha Magesa alitakiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kwenda jela miaka 3 ambapo alikosa fedha hiyo pia, ametakiwa kurejesha Tsh. 250,000 alizopokea pamoja na Ardhi iliyouzwa irejeshwe kwa serikali ya kijiji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags