Mhubiri nchini Nigeria achomwa moto hadi kufa

Mhubiri nchini Nigeria achomwa moto hadi kufa

Watu wasiojulikana wamechoma moto makazi ya mhubiri wa kanisa Katoliki kaskazini magharibi mwa Nigeria. Wakati wa shambulizi hilo, Padre Isaac Achi alichomwa moto mgongoni akiwa hai hadi kifo na mwengine alipigwa risasi na kujeruhiwa alipojaribu kukimbia.

Padre Collins Omeh aliyenusurika na kifo alikimbizwa hospitalini kwa matibabu. Sababu za shambulizi hilo bado haijajulikana mpaka sasa. Saa chache baadaye, majambazi walifanya shambulizi jingine tofauti katika jimbo la Katsina, kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika tukio hilo, mhubiri alipigwa risasi na wengine watano walitekwa nyara, walipokuwa wakijiandaa kuhudhuria ibada ya Jumapili.

Aidha eneo la kaskazini mwa Nigeria lina wanamgambo wengi wenye misimamo mikali ya dini ya Kiislamu, ambao wamekuwa wakifanya machafuko ikiwemo utekaji nyara.

Machafuko hayo yamezidisha wasiwasi huwenda uchaguzi wa Rais ambao umepangwa Februari 25, hautafanyika katika baadhi ya maeneo.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post