Mganga wa kienyeji ashikiliwa na polisi kwa kusababisha kifo cha mtoto

Mganga wa kienyeji ashikiliwa na polisi kwa kusababisha kifo cha mtoto

Jeshi la Polisi mkoani Lindi linamshikilia mganga wa kienyeji, Jalina Juma kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto, Yusufu Salumu (9), mkazi wa mtaa wa Rutamba Manispaa ya Lindi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pilly Mande alidai Julai Mosi, 2023 katika kijiji cha Rutamba Wilaya ya Lindi, mtoto huyo alipelekwa na wazazi wake nyumbani kwa mganga huyo wa kienyeji kwa lengo la kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa degedege uliokuwa unamsumbua.

Alisema baada ya kumfikisha kwa mganga huyo, alimlaza kwenye kitanda ambacho hakikuwa na godoro na kisha chini aliweka nyasi na kuziwasha moto uliosababisha kumuunguza sehemu za mgongoni na kumsababishia majeraha yaliyosababisha kifo.

Mande alisema baada ya tukio hilo, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi, Sokoine na Julai 8, 2023 ambapo alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu. Huku Jeshi la Polisi linamshikilia mganga huyo kwa mahojiano zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags