Mgahawa wapata umaarufu baada ya Lamar kuutaja

Mgahawa wapata umaarufu baada ya Lamar kuutaja

Mgahawa mmoja uliyopo Toronto nchini Canada uitwao ‘New Ho King’ umepata umaarufu na kuwa na wateja wengi baada ya ‘rapa’ Kendrick Lamar kuutaja kwenye ngoma yake ya ‘Euphoria’ ambayo aliitoa kwa ajili ya kumjibu Drake.

Kupitia wimbo huo Lamar aliutaja mgahawa huo kuwa na vyakula vizuri vya Kichina ambapo baada ya kutoa wimbo huo haikuchukua muda mrefu kwa mgahawa huo kutrend huku ukitajwa kukaribia hadhi ya nyota tano kwa mujibu wa Google.

Ngoma ya ‘Euphoria’ iliachiwa siku mbili zilizopita ambapo Lamar aliutoa wimbo huo kwa ajili ya kumjibu Drake ikiwa ni muendelezo wa bifu lao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags