Mgahawa unaotoa punguzo la bei kutokana na ukubwa wa mwili wa mteja

Mgahawa unaotoa punguzo la bei kutokana na ukubwa wa mwili wa mteja

Katika biashara kila mtu hutumia njia yake kuwavuta wateja, na wakati mwingine wamiliki wa bishara hulazimika kupunguza bei au kuboresha bidhaa zao ili waweze kupata wateja wengi zaidi.

Katika maeneo mengi ya migahawa imezoeleka wateja hupewa ofa kama vile wakinunua sahani zaidi ya moja ya chakula huongezewa na nyingine kama zawadi.

Jambo hilo limekuwa tofauti kwenye mgahawa mmoja uliyopo Malaysia ambao hutoa punguzo la bei kwa wateja kutokana na ukubwa wa mwili wa mteja, yaani wanaangalia unene na wembamba.

Katika mgahawa huo uliyojizolea umaarufu mkubwa unafahamika kama “Mongalian Master” wao wameamua kutumia njia ya kutoa punguzo kwa wateja kulingana na ukubwa wa mwili.

Ambapo kwenye mlango wa mgahawa huo umetengenezwa kwa kuwekewa njia za uwazi wa matobo mbalimbali yenye upana tofauti ambayo juu yake wameandika kila upana na kiasi cha pesa kitakachopungua.

Hivyo basi mteje hutakiwa kupita kwenye uwazi ambao utalingana na mwili wake, wembamba kuna uwazi wa kulingana na miili yao na matobo hayo ya kupita wembamba hutofautiana pia upande wa wanene pia ni hivyohvyo.

Mteja atapatapunguzo kulingana na tobo ambalo mwili wake utapita bila kukwama na punguzo huanzia asilimia 10,20,30,50, hadi 100, hivyo kulingana na ukubwa wa mwili wako ndiyo utapata kiasi fulani cha punguzo la bei, kwa wale wembamba sana ambao hupita kweye tobo la asilimia 100 hujikuta hadi wakila bure.

Vipi kwa huo mwili wako unadhani utatoboa kwenye hili?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post