Mfaume Mfaume pambano la marudiano na Pialali

Mfaume Mfaume pambano la marudiano na Pialali

Mabondia  wa Ngumi za kulipwa nchini wenye uhasimu mkubwa, Idd Pialali na Mfaume Mfaume jana Jumatano wamesaini mkataba wa pambano la marudiano linalotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu chini ya Kampuni ya Posh Queen Boxing Promotion.

Aidha hafla ya utiaji saini wa pambano hilo ilifanyika mchana wa jana kwenye viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam huku kila mmoja akitamba kumaliza pambano mapema.

Hata hivyo Pambano hilo lililopewa jina la King Of The Night linaloteka hisia za wengi kutokana na upinzani uliopo baina yao na kambi zao ambapo mabondia watapanda ulingoni kuwania mkanda wa Ubingwa wa kimataifa wa WBF katika pambano la raundi 12, uzani wa Super Walter.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post