Mfanyabiashara usikose app hizi kwenye simu yako

Mfanyabiashara usikose app hizi kwenye simu yako

Weeeeeuuuweeee! Haya sasa wale wafanyabiashara nina kikao na nyie kidogo, yaani nina jambo na nyie ndugu zangu. Kama mnavyo jua mimi na nyie ni damu damu, basi leo nimewajia na jambo muhimu ambalo litakufanya utusue katika biashara yako.

Jambo lenyewe sasa kwako wewe mfanyabiashara, nataka kukupa nondo za application ambazo zitakufanya uweze kukuza biashara na kukupatia wateja wengi zaidi.

Apps za mitandao ya kijamii (Whatsapp Business, Facebook, Instagram, Twitter, Telegram Na Tiktok); Ukishakuwa nazo, hakikisha unaziweka sehemu moja kwenye bio yako ili mteja wako aweze kukufollow sehemu zote.

Baadhi ya application zinazoweza kukuza biashara yako ni hizi hapa:


  1. App ya Canva

Hii itakusaidia kudesign na kutengeneza posts zako za kila siku za kupost kwenye akaunti zako mitandaoni. Ukiweza kutumia app ya CANVA, utapunguza gharama nyingi sana za kulipa graphics designer mara kwa mara kukutengenezea matangazo ya posts, utatengeneza mwenyewe posts za kuvutia sana kwa ajili ya kupost kwenye akaunti zako mitandaoni.

2. App ya KUZA business

Hii itakusaidia kutunza taarifa zako za biashara, kama mauzo pamoja na mipango yako ya biashara.

3. App ya BUFFER

Hii itakusaidia kuposti kipindi ambacho upo bize au hauna bando. Kupitia app ya BUFFER, unaweza kuandaa posts za kupost wiki nzima au mwezi mzima ukaweka na muda kisha muda huo ukifika posts hizo zitajiposti kwenye akaunti yako hata kama wewe upo bize. Hii inasaidia unakua active muda wote kwenye kuposti.

4. App ya VPN

Kuna kipindi internet inakua inasumbua kwasababu za kimazingira, mfano mwaka jana ilikua hauwezi kutumia Twitter Tanzania mpaka utumie VPN, hivyo kama ungekua unatumia Twitter kufanya biashara na hauna VPN, bila shaka biashara yako ingeathirika.

5. App ya SWAHILIESPAY

Kama una wateja nje ya nchi, basi hakikisha una download na unawasiliana na swahiliesapp ili uweze kutumia app yao kupokea malipo ya wateja wako wa nje.

6. MPESA APP, TIGO APP Na AIRTEL MONEY APP

Kama hauna akaunti ya benki bila shaka utashindwa kufanya matangazo ya Sponsored Ad kwani hautakuwa na njia ya kufanya malipo, lakini kama hauna akaunti ya benki lakini una app Ya AIRTEL MONEY AU MPESA, ni rahisi kutengeza kadi ya benki (Virtual mastercard) kupitia Mpesa yako au Airtel Money yako na kisha kufanya malipo ya Sponsored Ad bila kuwa na akaunti ya benki.

7. App ya ENPASS
 

App hii itakusaidia kutunza password zako za akaunti zako zote sehemu moja, inakusaidia kutunza kumbukumbu maana huwezi kukumbuka zote so ni muhimu kuwa nayo katika siku yako.

Uwiiiiiiih! Ubaki wewe tu kulifanyia kazi swala hili ili uweze kutusua katika biashara zako mwanangu sana, si unajua hatushindwani katika hili, fanya kudondosha comment yako hapo chini kama umeuelewa mzigo huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags