Mfahamu Nyoka anayeigiza kufa, Anapohisi hatari

Mfahamu Nyoka anayeigiza kufa, Anapohisi hatari

Kama tunavyojua hakuna jambo kubwa kama kuwa hai, katika kuhakikisha uhai wao unaendelea, nyoka aina ya ‘Eastern hognose snake’ wanaopatikana zaidi Amerika ya Kusini na nchini Canada huigiza kama wamekufa ili kujilinda dhidi ya binaadamu na maadui wengine.

Nyoka hao ambao jina lao la utani huitwa ‘zombie snake’ kwa mujibu wa tovuti ya #CBS wana sumu ambayo haina madhara kwa binadamu na mara chache sana kumgonga mtu, na wanapoona hatari kutoka kwa binadamu huigiza kama wamekufa kwa kulala chali huku wakiachia midomo wazi na mara baada ya hatari hiyo kuondoka hurudi katika hali ya kawaida.

Mbali ya njia hiyo pia nyoka hao hutumia mikwara kwa kuwatishia watu kwa kusimamisha nusu ya miili yao na kutunisha sehemu ya chini ya kichwa ingawa huwa hawafanyi mara nyingi sana.

Aidha kwa kawaida nyoka huwa wanatabia ya hujitetea au kujihami kwa kumgonga adui yao na kumpa sumu ambapo baadhi ya nyoka kama aina ya koboko huwa na sumu kali na huwa inachukua muda mchache kwa kiumbe kinachogongwa kupoteza maisha.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post