Mfahamu mwanaume aliyetengwa baada ya kupona kwenye ajali

Mfahamu mwanaume aliyetengwa baada ya kupona kwenye ajali

Siku zote waswahili wanasema ukistajaabu ya Musa utayaona ya Firauni, msemo huo ulijionesha kwenye historia ya ajali ya kuzama kwa meli ya Titanic, iliyotokea Aprili 14, 1912 Southampton, nchini Uingereza.


Ambapo katika ajali hiyo inayoendelea kutajwa kwenye kumbukumbu za kihistoria takribani watu 700 walifanikiwa kutoka wakiwa hai na kupokelewa vizuri katika mataifa yao, lakini kwa manusura Masabumi Hosono ambaye ni raia pekee wa Japan, aliyepona kwake ilikuwa tofauti kwani baada ya kurudi nchini kwao alifukuzwa kazi, alitengwa na kutuhumiwa kwa nini alipona na hakufa kama abiria wengine.


Masabumi Hosono, alikuwa ni Afisa wa Serikali Nchini Japani alikuwa akifanya kazi Urusi kama Makamu wa Bodi ya Reli ya Wizara ya Uchukuzi, alikuwa ni miongoni mwa abiria wa kwenye meli hiyo ambao walikaa daraja la pili.



Kati ya watu waliofanikiwa kupona katika ajali hiyo Hosono alibahatika baada ya kupata nafasi katika 'boti' ndogo ya uokozi, na hapo ndipo alinuuru maisha yake.

Kutokana na kupona kwake alipofika nchini Japan mambo yalikuwa tofauti kabisa
alipokelewa kwa makaribisho yasiyofaa ambapo alikabiliwa na shutuma kali kutoka kwa jamii na vyombo vya habari ambavyo viliwalaani watu walioishi kama waoga na kusifu ushujaa wa wale waliofariki.


Kulingana na Metropolis ya Japan, Honoso alichukuliwa kama mtu ambaye hakuifuata kanuni ya "wanawake na watoto kwanza’’ iliyowekwa nchini humo huku wakidai kuwa manusura huyo aliepuka kifo cha heshima hivyo kupelekea kutengwa na jamii.


Licha ya kutengwa alifukuzwa kazi mwaka huo ingawa alikuja kuajiriwa tena baadaye, lakini aliishi kwa mateso na kunyanyapaliwa na kutengwa mpaka kifo chake kilivyotokea mwaka 1939 na hata baada ya kufariki sehemu aliyokuwa akiishi ilikatazwa mtu yeyote kufika.

Ikumbukwe kufuatia na ajali ya Titanic watu 1,500 walifariki na wengine 700 kupona/kunusurika na kifo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post