Mfahamu mwanaume aliyeacha kazi apate muda wa kuhudhuria misiba

Mfahamu mwanaume aliyeacha kazi apate muda wa kuhudhuria misiba

Linapozungumziwa suala la uraibu baadhi ya  watu hudhani jambo hilo linaishia tu kwenye kunywa pombe, kula, kuvuta sigara au usingizi, lakini ukweli ni kwamba uraibu upo kila mahali na katika vitu mbalimbali.

Ukiachana na hao wenye uraibu wa ulevi au kula, fahamu kuwa yupo mwanaume aliyeathirika na tabia ya kupenda kuudhuria kwenye mazishi, hadi kupelekea aacha kazi apate muda wa kutosha wa kwenda kwenye mazishi.

 Mwanaume huyo anafahamika kwa jina la Luis Squarisi kutoka mji wa Batatais, Brazil ambaye anauraibu huo wa kupenda kuhudhuria mazishi.

Inaelezwa kuwa baada ya kifo cha baba yake aliyefariki mwaka  1983, ndipo Luis alijikuta akianza tabia hiyo ya kushangaza.

Na katika ukuaji wake aliendeleza jambo hilo hadi kufikia mbali zaidi kwani amewahi kuweka wazi kuwa aliacha  kazi yake ili apate muda mwingi wa kuudhuria kwenye mazishi mbalimbali.

Jambo hilo limekuwa la kawaida na kumpelekea kupata umaarufu kwenye mji wa Batatais, kwani watu wamejikuta hawatamani Luis apate matibabu ya kuondokana na shida hiyo.

Kwani kila afikapo kwenye mazishi wanamuona kama faraja na wakati mwingine asipo onekana watu huuzunika zaidi.

Pia Luis amewahi kukiri kuwa kila siku akiamka anasikiliza redio kujua sehemu zenye msiba, ili aweze kuhudhuria na asiposikia kwenye redio hupiga simu hospitali kwa ajili ya kufahamu watu waliofariki.

Hivyo basi hujikuta akifik katika misiba mbalimbali hata ile ambayo hamfahamu mtu yeyote kwa ajili tu ya kufurahisha nafsi yake, na asipofanya hivyo hata kwa wiki moja tu hujikuta akihisi kuumwa kabisa.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags