Mfahamu Mwanamke Mwenye Wivu Zaidi Duniani

Mfahamu Mwanamke Mwenye Wivu Zaidi Duniani

Mfahamu Debbi Wood mwanamama kutoka nchini Uingereza anayetajwa kuwa mwanamke mwenye wivu zaidi duniani, kutokana na tabia yake ya kutomuamini mume wake Steve Wood.

Mwanamke huyo alipewa cheo hicho cha kuwa mwanamke mwenye wivu zaidi duniani kutokana na tabia yake ya kutumia vipimo vya uaminifu kama ‘Lie Detector Tests’ mara kwa mara kwa mumewe ili kuthibitisha kama mumewe hakuwa akimdanganya.

Mbali na kutumia vipimo hivyo pia mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kukagua vifaa mbalimbali anavyotumia mume wake ikiwemo Simu, Kompyuta, Barua pepe anazozipokea, marafiki anaoongozana nao huku akimpiga marufuku kutazama wanawake kwengine kwenye runinga na magazeti.

Tabia hiyo ya kuwa na wivu kupitiliza imehusishwa na ugonjwa wa kisaikolojia unaojulikana kama ‘Othello Syndrome’ ambao husababisha mtu kuwa na fikra au mawazo ya uongo bila kuwa na ushahidi wowote.

Licha ya changamoto hizo, Debbi na Steve wametajwa kuwa na ndoa iliyoimara na yenye kuvutia watu wengi zaidi, wawili hao walifunga ndoa mwaka 2014.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags