Mfahamu mwanamke aliyetumia nguo ya ndani moja hadi kifo

Mfahamu mwanamke aliyetumia nguo ya ndani moja hadi kifo

Waswahili wanasema ‘Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni’ msemo huu unatupeleka moja kwa moja kwa mwanamama Hetty Green, mwanamke ambaye ameishi akivaa nguo ya ndani (chupi) moja toka akiwa na miaka 16 mpaka umauti ulipomfika.

Hetty Green ni binti pekee wa mfanyabiashara kutoka Marekani aliyezaliwa 1834 aliyekadiriwa kumiliki utajiri wa dola 2.3 bilioni na kushika rekodi ya dunaia ya Guiness kuwa tajiri mbahiri zaidi kuwahi kutoke.

Akiwa na miaka 16 alishona chupi kwa mkono wake ambayo aliivaa mpaka umauti ulipomfika, huku kuhusu mavazi yake aliliripotiwa kuvaa koti moja jeusi ambalo alilibadilisha baada ya kuchakaa.

Licha ya kupata mume mwenye utajiri kama wake lakini tabia ya ubahili ilidaiwa kuwepo kwenye damu kwani aliendelea kuishi maisha duni kwa kula vyakula vya bei ya chini na vilivyolala, tabia hiyo ilipelekea kuleta matatizo katika familia yake.

Ambapo aliwahi kusababisha mwanaye kukatwa mguu kwa sababu ulipovunjika alichelewa kupatiwa matibabu kutokana na mama yake huyo kuhofia kutumia pesa zake katika matibabu hayo.

Hetty Greene alifariki mwaka 1916 akiwa na umri wa miaka 81 katika jiji la New York, na aliingizwa kwenye Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness kama "mtu tajiri na mbahiri zaidi duniani’.

Sababu ya kifo chake ilikuwa kiharusi kilichotokana na ugomvi wake na mfanyakazi wake wa ndani ambapo mfanyakazi huyo aliomba kuongezewa mshahara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags