Mfahamu kikongwe anayetibu na kusafisha macho kwa ulimi

Mfahamu kikongwe anayetibu na kusafisha macho kwa ulimi

Na Asma Hamis 

Wakati baadhi ya watu wakienda kwenye vituo vya huduma za afya kupatiwa matibabu ya macho pale yanapopata matatizo, hiyo ni tofauti katika kijiji cha Crnjevo Kaskazini mwa Bosnia kwani baadhi ya watu wamekuwa wakikimbilia kwa kikongwe Hava kwa ajili ya kusafishwa macho kwa kutumia ulimi.

Hava Cebic maarufu kama "Bibi Hava," mwenye umri wa miaka 80 amekuwa akitumia njia ya kipekee ya kuwasafisha watu macho kwa kutumia ulimi wake kwa takribani miaka 40.



Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Deccanchronicle’ imeeleza kuwa bibi huyo mwenye kipaji cha kipekee amekuwa akitumia muda wake mwingi katika kusafisha macho ya watu kwa kutoa uchafu kama vipande vya chuma, mchanga, mbao, mkaa, vioo na vumbi kwa kutumia ulimi.

Inasemekana kuwa bibi huyo aligundua kipaji hicho miaka mingi iliyopita baada ya kumponesha kaka yake aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya macho kwa muda mrefu.

Kabla ya kuanza matibabu hayo Hava huzingatia usafi wake wa kinywa ambapo hutumia pombe ili kuzuia maambukizi kwenye jicho, huku akikadiriwa kuwapatia matibabu zaidi ya watu 5,000 wakiwemo wageni kutoka sehemu mbalimbali.

Tiba hii ya maajabu hugharimu takriban dola 14.20 za Kimarekani ikiwa ni sawa na Tsh 37,000, licha ya kuwa ni msaada kwa watu lakini matitabu hayo hayajafanyiwa majaribio ya kitaalamu kama kweli yanaponesha matatizo ya macho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags