Mfahamu John anayetengeneza viungo bandia

Mfahamu John anayetengeneza viungo bandia

Mwanaume mmoja kutoka nchini Nigeria aitwaye John Amanam, amewashangaza wengi kupitia mitandao ya kijamii kutokana na ubunifu wake wa kutengeneza viungo bandia vya ngozi nyeusi.

John ambaye ni mhitimu wa ‘kozi’ ya Sanaa na Viwanda kutoka Chuo Kikuu cha Uyo ni Muafrika wa kwanza kuzalisha viungo bandia vya watu ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili kutokana na sababu mbalimbali.

Baada ya mdogo wake kupoteza mguu alipopata ajali ya gari mwaka 2018 familia yake iliamua kuagiza kiungo bandia kutoka nje ya nchi, lakini baada ya kuwasili hakikulingana na rangi ya ngozi ya mdogo wake, ndipo wazo la kusomea shahada ya Sanaa lilipomjia na kupelekea afungue kumpuni ya ubunifu akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Immortal Cosmetic Art’.

Kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni aliweka wazi kuwa yeye hutengeneza viungo mbalimbali vya mwili vikiwemo masikio, pua, matiti, mikono, vidole, miguu na vinginevyo kwa lengo la kuwapa faraja waliopata ulemavu huku akiondoa unyanyapaji kwa umma.

Viungo anavyotengeneza John vinatajwa kuendana kabisa na ngozi halisi ya binadamu hivyo basi si rahisi mtu kugundua kuwa kiungo ulichonacho ni bandia






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags