Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) inayosimamia ulinzi wa taarifa binafsi kutoka Nchini Ireland (DPC) imechukua uamuzi wa kuwapiga faini ya trillion 3 kampini ya META baada ya kampuni hiyo kukiuka agizo la kutohamisha data za watumiaji wa Facebook kwenda Marekani.
META ilipewa miezi 5 kusitisha uhamishaji wa taarifa binafsi za watumiaji wake ikiwa ni utekelezaji wa zuio la Mahakama ya EU lililotolewa mwaka 2020 dhidi ya kampuni zinazochakata na kuhifadhi taarifa binafsi.
Mpaka sasa, META imefikisha faini za Tsh. Trilioni 5.9 kutokana na ukiukaji wa kanuni ya jumla ya ulinzi wa 'Data' ya umoja wa Ulaya (GDPR), iliyoanzishwa mwaka 2018.
Leave a Reply